Mchekeshaji wa kundi la Orijino Komedi, Masanja Mkandamizaji amefunguka na kuzungumzia jinsi alivyoupata uchungaji wake.
Masanja ambae kwa sasa anaendesha huduma ya ‘Street Gospel’, amekiamba kipindi cha Uhondo cha EFM kuwa imani yake ndio imemfanya kuwa mchungaji.
“Uchungaji upo wa aina mbili, kuna wa kuoteshwa na wakusomea. Kwa mfano ukiangalia mapadri wa Roman hakuna Padri aliyeoteshwa, wote wamesomea. Hata mimi sasa hivi nasomea uchungaji, lakini pia mimi nimekuwa nikiishi maisha ambayo yamenipelekea kuwa hivi, Kanisa lilikuwa ni sehemu ya maisha yangu, kabla ya kuokoka na baada ya kuokoka,” alisema Masanja.
Aliongeza, “Hudama yangu ambayo naiendesha sasa hivi ni Street Gospel na kazi yetu sisi ni kuhubiri mitaa ya mungu, kwa hiyo tunahubiri kwenye mitaa ya ulimwengu. Pia tuna kanisa letu linaitwa AGT lipo Kariakioo,”