Mtangazaji mkongwe nchini, Gadner G Habash, amerejea tena kwenye kituo chake cha awali, Clouds FM.
Gadner akisaini mkataba wa kujiunga tena na Clouds FM. Aliyeinama ni Meneja wa Vipindi wa kituo hicho, Shafii Dauda |
Gadner anajiunga tena na redio hiyo akitokea EFM alikokuwa akifanya kipindi cha jioni cha Ubaoni. Kabla ya EFM, Gadner alikuwa mtangazaji wa kipindi cha Maskani cha Times FM. Mtangazaji huyo anatarajiwa kurejea kwenye kipindi chake cha jioni, Jahazi.
Mtangazaji huyo anayejulikana kwa jina la utani ‘Captain’, anaingia kwenye kikosi cha Clouds FM ambacho hivi karibuni kilipata pigo baada ya watangazaji wake wawili, Gerald Hando na Paul James kuacha kazi. Wawili hao wanadaiwa kujiunga na EFM hivi karibuni.