Lulu amesema kuwa haamini ushirikina wala hajawahi kufanya kazi yoyote katika ushirikina kuanzia utoto wake.
Amefunguka hayo usiku wa kuamkia jana kupitia Friday Night Live ya EATV na EA Radio baada ya kuulizwa kuhusiana na comment zinazo endelea kwenye mitandao ya kijamii kuwa ushindi wa tuzo yake umetokana na ushirikina.
Lulu alifunguka kuwa kuanzia utoto wake amekuwa akiishi katika maisha ya uigizaji hivyo kila kitu kimepangwa na ndiyo maana amefanikiwa kufika hapo alipo.
Lulu ameiambia FNL “watu kama hawapendi maendeleo yako ni lazima wataongea lolote kuhakikisha kuwa wanakusema tu pale unapo fanikiwa”.
Hata hivyo msanii huyo aliamua pia kufungukia kuhusiana na mahusiano yake na mama mzazi wa marehemu Kanumba baada ya mama huyo kutoonekana kwenye kumpokea msani huyo ilihali mama huyo amehusika kwenye filamu iliyo mpa Lulu ushindi huo.
Lulu amesema hana tofautioi yoyote na mama huyo bali inawezekana alitingwa na shughuli za kimaisha na ndiyo maana hakuweza kwenda kumpokea uwanja wa ndege wa Mwl Julius Kambarage Nyerere.
Hataivyo alisema huwa wanawasiliana naye kwa simu japokuwa sio mara kwa mara.
Kuhusu uwepo wa mahusiano ya kimapenzi kati yake na Majay, Lulu alisema hawezi kuongelea suala hilo kwa kuwa bado mambo hayajafikia hatua nzuri.
“Siwezi kusema lolote kwa kuwa naweza kusema kuwa ni kweli, lakini ikawa si kweli na pia naweza kusema si kweli na ikawa kweli ” Alisema Lulu.