Sakata la Makamba na Muitaliano Lachukua Sura Mpya


Sakata la Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira na Muungano), January Makamba na Mdogo wake Mwamvita kudaiwa kupokea rushwa kutoka kwa raia wa Italia, Vincenzo Cozzolino ili wamsaidie kupata zabuni ya ujenzi limechukua sura mpya.

Sauti na jumbe mbalimbali zilizosambazwa na kuwekwa kwenye mtandao na mmiliki wa tovuti ya U-Turn, Mange Kimambi, raia wa Tanzania aishie Marekani, zinaonesha mazungumzo kati ya watatu hao, mwaka 2011. Jana, Mwamvita na Makamba walikiri kuwa sauti hizo ni za kweli.

Msikilize Mhe. January Makamba akifunguka kuhusu sakata hilo hapa chini:



Muitaliano huyo ambaye anadaiwa kumpa Mange Kimambe ushahidi wote wa mawasiliano kati yake na Ndugu hao, amejitokeza na kuwasafisha akidai kuwa hakuwahi kuwapa rushwa wala kuhusiana na January kibiashara.
Cozzolino ameandika ujumbe akidai kuwa ingawa yeye na Mwamvita walikuwa na uhusiano wa mapenzi mwaka 2011 na baadaye kujiingiza katika biashara binafsi ambayo ilipelekea kugombana kwao, hawakumhusisha January kwa aina yoyote katika biashara yao.
“Sikuwahi kumuomba [January] kunisaidia katika biashara zangu. Sikuwahi kumpa fedha. Mara chache nilizokutana naye ilikuwa ni mazungumzo ya kawaida ya kijamii. Nilikuwa na uhusiano na Mwamvita. Uhusiano wetu ulikuwa bomba mwanzoni lakini ukawa na mwisho mbaya,” ameandika Cozzolino.
Mwamvita.
Mwamvita Makamba.
Awali, sauti ya January na mwandishi wa habari iliyosambazwa, January anasikika akieleza kuwa aliwahi kukutana mara moja Dubai na Muitaliano huyo na kwamba alitambulishwa kama mpenzi wa dada yake.
Alisema baadaye dada yake alimwambia wameanza kufanya biashara ya kahawa na Muitaliano huyo na baadae biashara hiyo kufa huku ikiwaacha katika mzozo.
Kwa mujibu wa Kamambe, Muitaliano aliyekuwa ameweka nusu ya mtaji ambayo ni dola milioni 50, alianza kudai kiasi hicho cha fedha na sio vinginevyo.
Ufuatao ni ujumbe alioandika Vincenzo Cozzolino ukionyesha kuwa January Makamba hausiki na sakata lao:
barua
Alisema kuwa awali, Muitaliano huyo alikuwa anajaribu kumshawishi Mwamvita amkutanishe na viongozi wakubwa wa serikali ikiwa ni pamoja na Katibu Mkuu.
Hata hivyo, Mange Kimambe ambaye ndiye anayeeleza kuwa na nyaraka zote za ushahidi aliokabidhiwa na Muitaliano huyo na kwamba hivi sasa Muitaliano amelipwa na kukubaliana kumsafisha Mbunge huyo wa Bumbuli.
Mange amesisitiza kuwa ana ushahidi wote wa January na dada yake kupokea rushwa kutoka kwa mfanyabiashara huyo na yuko tayari kuwakabidhi Takukuru.

Sakata la Makamba na Muitaliano Lachukua Sura Mpya Rating: 4.5 Diposkan Oleh: Admin