AJIRUSHA KUTOKA GHOROFA YA 9 HOTELINI KARIAKOO


Muda mfupi uliopita,Mtu mmoja alietambulika kwa jina la Shirima ambaye ni Mfanyabiashara katika moja ya Maduka ya Kariakoo jijini Dar es Salaam,amejirusha toka ghorofa ya 9 ya Hoteli ya Concord iliopo Maeneo ya Kariakoo jijini Dar es Salaam na amekimbizwa hospitali kwa uangalizi zaidi maana haijafahamika kama kapoteza Maisha au bado yu hai.

Mfanyabiashara huyo alijirusha toka ghorofani na kuangkia katika Gari aina ya Toyota Corolla ambayo ni taxi iliyokuwa imepaki nje ya hoteli hiyo,chanzo cha kujirusha kwa mfanyabiashara huyo bado hakijafahamika mpaka sasa.

Mashuhuda wa tukio hilo lililotokea muda mfupi uliopita,wanaeleza kuwa walipatwa na mshtuko baada ya kusikika kishindo cha kitu kilichokuwa kimeangukia gari hilo na waliposogea kushuhudia ndipo walipobaini kuwa alikuwa ni mtu huyo alietambulika kwa jina moja la Shirima.
AJIRUSHA KUTOKA GHOROFA YA 9 HOTELINI KARIAKOO Rating: 4.5 Diposkan Oleh: Unknown