Heshima kwenu wakuu,
Nina mke na watoto wawili na ndoa yangu sasa inakaribia kufikisha miaka
6. Tulipooana tulikuwa tukiishi kwa amani na upendo lakini baada ya
kupata mtoto wa pili hali ikabadilika gafla akawa jeuri, majibu ya mkato
na kiburi, kila nikijaribu kumsihi na kukaa naye kujadili anatulia siku
moja au mbili baadae anarudia kama mwanzo.
Tabia zake zimenifanya niwe mkali na mimi kama kujihami na matatizo haya.
Nilienda kuomba ushauri kwa wataalam wa mahusiano wakaniambia nikae nae
tudiscuss na kama anatumia dawa za mpango wa uzazi aziache maana wakati
mwingine husababisha hasira za mara kwa mara na wakaniambia pia
nichunguze pia labda anaweza kuwa na mshikaj nimejarib kuchunguza hilo
nimeona hana.
Pia hata dawa za uzazi wa mpango aliziacha sasa anakaribia miez sita
anatumia mbinu za kiasili lakini ktk yote hayo bado habadiliki natamani
kuachana nae lkn nawaonea huruma sana wanang wataish ktk mazingira
mabaya na hata yeye tumetoka mbali sana nae,pia hata nikiachana nae
sitaman kuoa tena, zaid nawaona wanawake wote wako hivyo.
Naomba ushauri wakuu. Asante!