Wema Sepetu: Ningekuwa na uwezo wa kuzaa ningekuwa nimezaa muda mrefu sana

Mrembo mwenye ushawishi mkubwa zaidi kwenye social media hapa Bongo, ambaye alishawahi kujinyakulia taji kubwa zaidi la ulimbwende hapa Bongo bibie Wema Sepetu ameandika maneno mazito sana kwenye mtandao maarufu wa Instagram ambayo yamevuta hisia za watu mbali mbali wakiwemo ma superstar wengine ndani ya Bongo.


Mrembo huyo ameandika maneno yafuatayo kama yanavyoonekana kwenye picha hapo juu:


Ningekuwa na uwezo wa kuzaa ningekuwa nimezaa muda mrefu sana... But sina... Na siwezi kumkufuru mwenyezi mungu.... Au mngependa niwe nawaambia jinsi ninavyo hangaika usiku na mchana kupata mtoto wangu mwenyewe... Is dat wat u want...? kila ntakachofanya kwa ajili ya tumbo langu basi nitangaze... Au mnadhani siumii mnavyosema kuhusu maswala ya mtoto😞😞😞... Kumbukeni na mimi pia ni binaadam... Nina moyo kama nyie... Au mnadhani napenda kuona wenzangu wana watoto au wana ujauzito alafu mimi sina hata wa kusingiziwa... Mnaona nafurahia sio.... Hivi mna nini jamani... Yaani mtu unaweza weka post kwa nia nzuri then people jus come from nowea wanaanza kukuandikia maneno ya kukuumiza kabisa nafsi hadi mtu unakaa unajiuliza umemkosea nini mwenyezi Mungu... Kwani kuna niliemkosea yoyote mpaka muanze tu kunikashif na kunitolea maneno mazito namna hio... Kisa mtoto... Mnadhani naipenda hii hali... Hata mimi natamani kuitwa mama na hakuna kinachoniuma kama hicho.... So mnadhani sijui kama umri unaenda na maisha yenyewe sikuhizi mafupi anytime we die... Mnafikiria nisingependa kuacha hata ka copy kangu siku ndo Mungu anasema ananichukua... Hata mimi natamani ningekuwa napiga picha niko na mwanangu... I want dat with all my life but I cant.... Sitokaa nimkufuru Mungu wangu hata siku moja maana sijui ni kitu gani kaniandikia... But just dont rub it in... It hurts... And im jus a human being like each and everyone of u.... πŸ˜”πŸ˜”πŸ˜”
Mastaa wengine akiwemo mwanadada Mboni nao hawakukosa la kuandika katika kumtia moyo Wema Sepetu:


NIMEGUSWA 😑😑😑😫😫😫Pole sana mdogo wangu @wemasepetu @wemasepetu @wemasepetu @wemasepetu nimeona post yako na imeniuma sana, lakini naomba nikusihi kidogo " @wemasepetu Binadamu huwezi wakataza kasema, chukua mfano kwangu! Mimi nilisemwa sana kuwa mimi MGUMBA mimi siwezi zaa na maneno mengi tu ya kashfa na YA kuzaliliswa, bila ya wao kujua ni kiasi gani nilikuwa nasali usiku na mchana ili nipate mtoto wangu. Lakini Mimi wala sikuwajali hao walimwengu wanasema nini, niliendelea kumlilia MUNGU Wangu na mwisho wa siku alinipa HITAJI langu.. ALHAMDULILLAH πŸ™πŸ™ Wako wapi leo walionisema vibaya?! Wanajisikiaje ndani YA nafsi zao?? @wemasepetu mimi binafsi nimetafuta mtoto kwa miaka mingi sana, lakini siku Mungu alipotaka alinipa bila YA kutegeme..Mimi nimepata ujauzito nikiwa na miaka 35 y wewe upate tabu na kusononeka wakati hata 30th hujafika Mdogo wangu??!!USIISHI KWA AJILI YA WANADAMU, WAO SIO MIUNGU BWANA.. WEWE ENDELEA KULIA NA MOLA WAKO ATAKUJIBU TU. MUNGU ANAJIBU MDOGO WANGU.. TATIZO LETU SISI WANADAMU HATUNA INNA LLAH MASWABIRINA # SUBIRA KWETU HATUNA # Lakini jua MUNGU atakupa muda wako utakapofika. Wala usisononeke mbona flan ana mimba y wewe! NNA IMANI KABISA WAKATI WAKO BADO HAUJAFIKA , UKIFIKA UTAPATA TU UJAUZITO ENDELEA KUMUOMBA MUNGU TU NA WALA USICHOKE KUMUOMBA.. NA INSHAALLAH NTAKUWEKA KWENYE SALA ZANGU ZA KILA SIKU.. Wewe RELAX kwa kujua siku yako ipo tu.. Love you so much Dogo ake @wemasepetu ❤️πŸ˜πŸ˜˜πŸ™πŸ™NAJUA INAUMA SANA NA KUKERA HASWA. WANADAMU HEBU TUMUOGOPE MUNGU JAMANI HAPA TUNAPITA TU KUNA MOTO HUKO TUNAKO KWENDA.. ALLAH AKBAR πŸ™πŸ™πŸ™πŸ™ cc @chantelle8888 @martinkadinda @wemasepetu @petitman_wakuache @millytz1
Na sisi timu ya Mpekuzi Huru BLOGSPOT tunapenda kumtia moyo Wema Sepetu aelewe kwamba watoto ni zawadi kutoka kwa Mungu, hivyo asikate tamaa, azidi kumwomba Mungu, na kwenye maombi yake amwombe Mungu ampe Mume kwanza, akishakuwa na Mume wake ambaye anafahamika kwamba ni wake rasmi kabisa na Mungu naye atafanya kinachofuata ambacho ni kupanda mbegu za mtoto tumboni mwake.

Source: INSTAGRAM DOT COM
Wema Sepetu: Ningekuwa na uwezo wa kuzaa ningekuwa nimezaa muda mrefu sana Rating: 4.5 Diposkan Oleh: Mpekuzi Huru