Mauaji, mashambulizi ya kudhuru mwili na uporaji vimeendelea kuchafua taswira ya Tanzania baada ya juzi, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), kuuawa kwa kupigwa risasi na watu ambao hawajafahamika, raia wawili wa Uingereza kumwagiwa tindikali na mfanyabiashara kuporwa zaidi ya Sh40 milioni. 


Jana, Rais Jakaya Kikwete alikwenda Hospitali ya Aga Khan kuwajulia hali raia hao wawili wa Uingereza waliomwagiwa tindikali huko Zanzibar, Kate Gee (18) na Kirstie Trup (18) akisema tukio hilo limetia aibu kwa mataifa ya nje na kuliamuru Jeshi la Polisi kuhakikisha linawakamata na kuwafungulia mashtaka wote waliohusika.Mauaji

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Camillius Wambura alisema jana kuwa mauaji ya Mhadhiri huyo Msaidizi katika Idara ya Uhandisi na Teknolojia, Patrick Rweyongeza (32) yalitokea juzi saa saba mchana maeneo ya Magomeni Tanesco, Dar es Salaam, wakati marehemu alipokuwa ndani ya gari lake akielekea katikati ya jiji.

 

“Alipofika maeneo hayo alivamiwa na watu waliokuwa kwenye pikipiki aina ya Boxer ambao walimpiga risasi ya kifua upande wa kulia kisha kutokomea.”
 

“Baada ya kupigwa risasi alipelekwa Muhimbili lakini kabla ya kuanza kupatiwa matibabu alifariki dunia,” alisema Kamanda Wambura.
 

Alisema hakuna mtu yoyote aliyekamatwa kuhusiana na tukio hilo. “...Tunaendelea na upelelezi kufahamu tukio hilo lililofanywa na watu hao kama ni la ujambazi au kisasi.”

 

Akizungumza nyumbani kwa mjomba wa marehemu Mbweni, Dar es Salaam jana, Mkuu wa Idara ya Uhandisi, Dk John Mahunza alisema Rweyongeza alikutwa na mkasa huo baada ya kutoka benki kuchukua fedha kwa ajili ya shughuli za ofisi.

“Baada ya kuchukua fedha hizo Ubungo, alipanda gari kuelekea Magomeni na kufika maeneo ya Tanesco, walimzingira na kumlazimisha kufungua mlango, lakini aligoma na wakampiga risasi,” alisema.
 

“Baada ya kumpiga risasi mkononi, walimpora bahasha iliyokuwa na fedha... nadhani wale walikuwa wanamfuatilia tangu alipokuwa benki hadi anatoka.


Wasifu
 Dk Muhunza alisema marehemu alipata shahada yake ya kwanza mwaka 2004 chuoni hapo na baadaye shahada ya uzamili katika chuo kimoja cha London, Uingereza. Alifundisha chuoni hapo masomo ya Numerical Method na Building Design kwa miaka mitatu.
“Marehemu alikuwa na mpango wa kwenda kuchukua shahada ya uzamivu katika chuo kimoja London na alikuwa hajaoa.”
Msemaji wa familia, Damas Kayanda alisema marehemu anatarajiwa kuagwa leo kwa shughuli za ibada kufanyika katika Kanisa la Mtakatifu Raphael na kesho utasafirishwa kwenda Tabora kwa maziko.
Tindikali
Wasichana hao wawili walimwagiwa tindikali katika maeneo ya Mji Mkongwe wakiwa katika matembezi ya kawaida juzi usiku.
 
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Mkadamu Khamis Mkadamu alisema tukio hilo lilifanywa na vijana wawili waliokuwa wakiendesha pikipiki aina ya Vespa.
Mkadamu alisema Wazungu hao walikuwa walimu wa kujitolea katika Shule St Monica, Tomondo, Zanzibar.
Alisema waathirika hao wamedhurika kiasi kikubwa katika maeneo ya kifua na mikononi na baada ya tukio hilo, walipelekwa Hospitali Kuu ya Zanzibar na baadaye kuhamishiwa Hospitali ya Aga Khan, Dar es Salaam kwa matibabu zaidi.

 
Mganga Mkuu wa Aga Khan, Dk Jaffery Dharsee alikataa kuzungumza chochote kuhusiana na hali za wasichana hao akisema hajapata ruhusa kutoka kwa ndugu wa familia.
Maofisa mbalimbali wa Ubalozi wa Uingereza nchini walifika hospitalini hapo kuwajulia hali wagonjwa hao.

Uporaji
Majambazi wanne walimvamia mfanyabiashara wa vifaa vya magari na kumpora zaidi ya Sh40 milioni alizokuwa akipeleka benki.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala, Marieta Minangi alisema tukio hilo lilitokea juzi saa nne asubuhi kwenye makutano ya Mitaa wa Livingstone na Kiungani, Dar es Salaam wakati mfanyabiashara huyo aliyefahamika kwa jina moja la Bupedra akiwa na dereva wake kwenye aina ya Toyota Hiace.


Alisema walipofika katika eneo hilo walivamiwa na watu wanne waliokuwa kwenye pikipiki aina ya Boxer na walisimamisha gari hilo kisha kupiga risasi moja hewani na kuvunja kioo cha dirisha cha mlango wa mbele kwa nondo na kumtaka Bupedra awape fedha hizo zilizokuwamo kwenye begi haraka.


“ Watu hawa walikuwa wanajua kila kitu kilichomo kwa sababu waliposimamisha gari walitaka wapatiwe fedha haraka na walipatiwa na kutokomea, “ alisema Kamanda Marieta.

 
Alisema polisi wanamshikilia dereva wa gari hilo kwa upelelezi wa tukio hilo ambalo hakuna mtu aliyejeruhiwa.
Imeandikwa na Talib Ussi, Zanzibar, Minael Msuya, Bakari Kiango na Daria Erasto Dar es Salaam.

Credit: MCL
filed under:

Njiwa akiwa na ujumbe wa barua kama inavyo onekana

Njiwa akiwa amedhoofu kwa Baridi akiwa katika choo cha wanaume

Hii ni sehemu alipokutwa Njiwa huyo

Majengo nje ya Ofisi ya Afisa Mwajiri

Baadhi ya wafanyakazi wakielekea eneo la tukio

Afisa Mwajiri (Mwenye shati ya bluu) Na baadhi ya wafanyakazi wakishuhudia tukio

Mashuhuda wakitoka eneo la tukio

Barua iliyoletwa na Njiwa maeneo ya Ofisi ya Mwajiri upande wa mbele na nyuma

Jengo la Ofisi ya Afisa Mwajiri

Stesheni ya TAZARA kituo cha Mbeya

WAFANYAKAZI wa Mamlaka ya Reli, kati ya Tanzania na Zambia(TAZARA) jana walijikuta katika wakati mgumu na baadhi yao kulazimika kuzikimbia ofisi zao, baada ya ndege aina ya njiwa kukutuwa katika moja ya choo cha ofisi hiyo akiwa amefungwa hirizi shingoni, huku akiwa na barua yenye ujumbe wa onyo kali.

Tukio hilo la aina yake, lilitokea mapema leo saa mbili asubuhi katika ofisi za mamlaka hiyo zilizopo eneo la Iyunga Mkoani hapa, hali ambayo mbali na baadhi ya wafanyakazi wake kuzikimbia ofisi, ilisababisha kuibuka kwa mjadala mkubwa dhidi ya tukio hilo.

Mtandao huu ulifanikiwa kushudia njiwa huyo mweusi akiwa nyuma ya choo cha kiume katika eneo hilo la ofisi ya mwajiri, huku akiwa amefungwa hirizi shingoni iliyozungushiwa shanga mchanganyiko wa rangi tatu, ambazo ni Nyekundu, Njano na Nyeupe.

Mbali ya kuwa na hirizi hiyo, pia njiwa huyo alikuwa amebeba barua inayodaiwa kuwa ni ya mmoja wa wafanyakazi wa Mamlaka hiyo (jina limehifadhiwa kwa sababu maalumu) ambaye anadaiwa hivi karibuni kufukuzwa kazi kwa makosa ya ubadhirifu.

Barua hiyo ilikuwa na maandishi mekundu yenye ujumbe ulioandikwa kwa lugha mbili za Kiswahili na kiarabu, ambapo katika maandishi ya Kiswahili yalisomeka “

Naomba majibu haraka kama mtarudisha binti huyu kazini” ilisema sehemu ya ujumbe huo, huku ikiwa na orodha ya majina matatu ya viongozi wa shirika hilo.

Mbali na ujumbe huo ukiwa umeandikwa kwa maandishi ya mkono yaliyokolezwa kwa wino mwekundu upande wa nyuma, lakini upande wa mbele kulikuwa na maandishi yakiwa ni barua ya kutaarifiwa kufukuzwa kazi kwa mfanyakazi huyo.

Akizungumzia tukio hilo, Mwajiri wa mamlaka hiyo kanda ya Mbeya, aliyejitambulisha kwa jina la Mchaba Mgweno, alikiri kutokea kwa tukio hilo na kwamba waliobaini ni wahudumu wa usafi.

Aliongeza kuwa baada ya kupokea taarifa hiyo aliwaarifu na wafanyakazi wenzake ambao walikusanyika na kumshuhudia Njiwa huyo mweusi akiwa amedhoofika huku akiwa na barua hiyo yenye vitisho.

Alisema baada ya kushuhudia hali hiyo waliamua kutoa taarifa kituo cha polisi kilichopo ndani ya shirika hilo, ambapo waliichukua barua hiyo na baadhi ya wafanyakazi hao wakienda kutoa maelezo kituoni hapo.

“Kwa kweli hali hii si ya kawaida, ila kwa sasa siwezizungumzia chochote kwa kuwa hata mimi tukio hili limeniweka katika wakati mgumu na nimeshindwa kuendelea na majukumu yangu ” alisema Mgweno.

Hata hivyo kuliibuka malumbano makali kati ya wafanyakazi wa shirika hilo walioshuhudia tukio hilo, ambapo baadhi yao wakidai kuwa tukio hilo ni la kutengenezwa kwa lengo la kuchafuana.

“Hebu angalia hiyo barua yenyewe mbona ni kivuli (Photocopy), kama ingekuwa ni ya ….wanamtaja mfanyakazi aliyefukuzwa jina limehifadhiwa ingekuwa ni nakala halisi….haiwezekani mambo haya ni kutaka kuchafuana tu” alisema mmoja wa wafanyakazi hao.

Lakini baadhi yao wakiamini kweli kuwa barua hiyo ilitumwa ili itoe vitisho kwa viongozi wa shirika hilo.

Baadhi ya askari polisi wa kituo cha Tazara walikiri kutokea kwa tukio hilo na kwamba wanaendelea na uchunguzi ili kubaini ukweli wake.

“Ndugu zangu nyie mnajua taratibu za utoaji wa taarifa kwa jeshi hili, maana wapo wahusika, lakini kwa kifupi sisi tulipokea taarifa na tunaendelea kuzifanyia kazi” alisema mmoja wa askari hao.

Hata hivyo, hadi tunapoondoka eneo la tukio majira ya saa sita mchana Njiwa huyo alikuwa bado yupo eneo la tukio.
filed under: ,
NI SIASA VS BONGO MOVIE


SHINDANO LIMEISHA KWA KUTOKA DROO


JACKLINE WOLPER ULINGONI
Mh. Nassari na mashabiki wengine wa Mh. Mdee wakiwa wamembeba bondia wao
Ni katika tamasha la matumaini 2013 Jackline Wolper na Halima Mdee walizipiga. Hata hivyo hapakupatikana mshindi baada ya kutoka Droo

MWANAFUNZI wa Chuo cha Ufundi (VETA), mkoani Dodoma, Taliki Juma (22), amefariki dunia baada ya kujilipua kwa mafuta ya petroli. Mbali na mwanafunzi huyo kufariki, watu wengine wanane waliokuwa karibu na moto huo nao walijeruhiwa vibaya.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma na kusainiwa na Kamanda wa Polisi wa mkoa, David Misime, tukio hilo lilitokea juzi saa 12.30 jioni katika Kitongoji cha Machaka, Kata ya Nzughuni.

Kamanda Misime alisema, katika tukio hilo marehemu alinunua mafuta ya petroli lita tano katika kituo cha mafuta cha Nanenane na kisha kujilipua.

“Juma ambaye ni mwanafunzi wa fani ya ufundi wa magari, alimwaga petroli hiyo ndani ya saluni ya Irene Mapunda na kujilipua.

“Watu waliokuwa karibu naye walijaribu kumsihi asijilipue lakini hawakufanikiwa, kwani aliwasha kibiriti ndani ya saluni hiyo na kusababisha moto mkubwa kulipuka ambao uliwaunguza wengine waliokuwa karibu naye pamoja na mali zote zilizokuwa ndani ya Saluni hiyo.

“Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa chanzo cha tukio hilo ni wivu wa kimapenzi, hata hivyo Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linaendelea na uchunguzi wa kina juu ya tukio hili,” ilieleza taarifa hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo waliojeruhiwa ni Mugina Hessein (32), Benson Mushi (11) Japhet Japhet (18), Meshack John (18), Swaibu Kassim (20),Ester Silau (30), Shaban Pili (20) na Fedrick Gabriel (21).

Majeruhi wote wamelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma (General) na tathimini ya hasara iliyosababishwa na moto huo bado haijafahamika.
filed under: ,
Mgambo wa jiji la Dar es Salaam wakiwa katika zoezi la kuwakamata Madada wanaofanya biashara ya kuuza miili yao wajulikanao kama Machangudoa katika eneo la Sinza.

Picha mbalimbali zikionyesha namna walivyokuwa wakipakiwa ndani ya Gari tayari kwa kupelekwa katika vyombo vya sheria
Changudoa akipanda kwenye gari 
Hapa akifanya vituko asikamatwe


Hapa wanaondoka nao
filed under: ,

Mimi ni dereva namuendesha mke wa boss wangu.  

Toka nimeanza kazi hii yapata mwaka mmoja sasa mke wa boss alianza mitego nikawa namvumilia, kuna siku tulisafiri kwenda Mtwara kwenye biashara za huyu mama, kufika kule yule mama alilipia chumba kimoja tu nakuniambia tutalala wote na nikikataa ndiyo itakuwa mwisho wa ajira yangu nikikubali atafanya mpango wa kumshawishi boss aniongeze mshahara, sikuwa na jinsi nikala mzigo bila hata ya condom basi ndiyo ikawa mchezo kila tukitoka lazima mama boss anipe mzingo na kiukweli mshahara niliongezewa.

Sasa jana aliniita nakunieleza kuwa yeye ni mjamzito na mimi ndiyo mwenye huo mzigo ila akanishauri niuchune kwa sababu mumewe anajua kwamba mkewe ni mjamzito.

SASA WASIWASI WANGU AKIJA KUZALIWA MTOTO ANAFANANA NA MIMI ITAKUWAJE?
NA BOSS YANGU NI AFISA USALAMA WA TAIFA.

Naomba ushauri waungwana.
filed under: ,

MSAIDIENI HUYU MSICHANA:
Pole na kazi Mpekuzi, Mimi ni msichana mwenye umri wa miaka 22, nina rafiki yangu ambaye nimesoma naye na ni kama ndugu yangu wa damu kutokana na tulivyo na watu wote wanajua kwamba mimi ni yeye na yeye ni mimi.
Rafiki yangu huyu nimesoma naye kuanzia O-leve, mpaka advance na sasa tupo wote chuo hapa dar  es salaam, kwa kifupu ni urafiki wa damu.

Mwaka jana katikati rafiki yangu huyu alinitambulisha kwa boyfriend wake ambaye ni kaka anayesoma chuo kingine ambacho hakiko mbali na chuo chetu, kwa kweli wanapendana sana na ni kaka mzuri sana ambaye rafiki yangu anajivunia kuwa naye, na kutokana na ukaribu wangu na rafiki yangu, nimekuwa nikiwasiliana sana na shemeji yangu huyu kiasi kwamba naye amekuwa ni mtu wa karibu sana, na muda wowote asipompata rafiki yangu amekuwa akinipigia mimi, na hata mara nyingine tumekuwa tukienda matembezeni watu watatu, yaani mimi rafiki yangu na shemeji, ukaribu nilionao na shemeji yangu huyu umenifanya nianze kumthamini na kumjali hadi naogopa, mara ya kwanza nilidhani ni kwa sababu nampenda rafiki yangu, lakini kwa sasa naona imepitiliza na nimegundua kwamba nampenda huyu kaka na natamani siku nifanye naye mapenzi sababu mimi nipo single kwa sasa kwakuwa nilikorofishana na aliyekuwa mpenzi wangu.

Hali imekuwa mbaya kwani hata sasa naona hata huyu shemeji yangu nae ananipenda lakini hawezi kuniambia, natamani siku aje hostel wakati huyu rafiki yangu hayupo ili alale hapa hapa. 

Kwa kweli nimechanganyikiwa kwa kifupi nahisi kuumwa kwa sababu nina mpenda kupita maelezo sema nahofia kumuumiza rafiki yangu kwani najua siku nikimpindua lazima shemeji amuache rafiki yangu aje kwangu sababu nina shepu ya kumtamanisha mwanaume yoyote.
Naombeni msaada wana jamii.

filed under:


Katibu Mkuu wa CCM ndg Abdulrahman Kinana amesema kinga ya Bunge isiwe sababu ya baadhi ya wabunge kutumia fursa hiyo kuchafua watu wasio na nafasi ya kujitetea ndani ya mhimili huo wa Dola.

Amehadharisha hayo alipozungumza na waandishi wa habari  mjini Dodoma juzi kukanusha tuhuma zilizoelekezwa kwake binafsi na chama chake na Kambi ya Upinzani Bungeni.

Tuhuma hizo zilihusu shehena ya pembe za ndovu iliyokamatwa Vietnam mwaka 2009 ambazo aliziita za kupika na za uongo. "Tuhuma hizo hazina ukweli wowote, zina nia mbaya dhidi yangu na zimelenga kuniharibia taswira yangu na ya chama changu," alisema Kinana.

Alisema hahusiki vyovyote na tuhuma hizo na kutuhumu Kambi ya Upinzani Bungeni kwa kushindwa kujadili hoja za maana za maendeleo na badala yake kujihusisha na siasa za kuchafua heshima za watu.

"Bado nina nguvu na sijayumba kwa namna yoyote. Nina jukumu la kuilinda CCM na kutekeleza ahadi tulizozitoa kwa wananchi kupitia ilani ya uchaguzi," alisisitiza na kushangaa suala hilo la tangu mwaka 2009, kujitokeza sasa.

"Jibu ni jepesi, lengo ni kumvunja moyo Katibu Mkuu wa CCM ambaye CHADEMA inamwona tishio kwao," alisema Kinana na kusisitiza kuwa tuhuma dhidi yake hazina msingi na hata kambi ya upinzani inatambua kuwa mamlaka zote za ulinzi na usalama za ndani na nje zilimsafisha.

Kinana alisema baada ya shehena hiyo kukamatwa, Mamlaka ya Kimataifa ya Kudhibiti Wanyama Walio Hatarini Kutoweka (CITES) na Polisi wa Kimataifa (INTERPOL) walifuatilia na wakabaini kuwa hakuhusika.

Watuhumiwa walikamatwa na kufikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, akiwataja kuwa ni Eladius Colonerio (Mkurugenzi wa Team Freight (T) Ltd), Gabriel Balua (Meneja wa TEA Freight (T) Ltd) na Shaban Yabula (Mkurugenzi Mtendaji wa Kigoma M.N. Enterprises (T) Ltd).

Wengine ni Erick Morand (Ofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania katika bandari ya Dar es Salaam) Issa Lweno, Norbert Kiwale na Abubakari Omar Hassan.

Kinana alikana kumiliki meli yoyote na wala kujihusisha na usafirishaji wa nyara hizo za Serikali. Katika mkutano huo, alimtuhumu Msigwa kuwa na ajenda ya siri na kswamba aliamua kumtuhumu huku akijilinda kwa kinga za Bunge na akijua kuwa kufanya hivyo ni kutumia vibaya kinga hiyo.

Kinana amesema anaamini chanzo cha kuchafuliwa kwake na wapinzani ni wadhifa wake.

Kinana alisema anaamini kuwa kama asingekuwa na wadhifa huo, asingesakamwa kwa tuhuma alizoziita za uzushi.

“Hivi vitu havinisumbui. Hapa tatizo ni kuwa Katibu Mkuu wa CCM. ‘I am a senior officer’ (Ofisa Mwandamizi) sasa katika chama changu kama ningekuwa nimekaa nyumbani nafanya biashara zangu yasingetokea haya.

“Nataka kuwaambia tu, waelewe kuwa hawawezi kunitoa katika ajenda yangu ya msingi. Hii ni sawa na mwanajeshi anayekwenda kupigana vita na adui halafu akawa na vikundi vidogo vinakushambulia kutoka kila upande kukutoa katika lengo la msingi... ni lazima mtu ukomae na ili ufanikiwe,” alisema Kinana.

Alisema Msigwa alikuwa katika Kamati ya Ardhi na Maliasili ya Bunge tangu mwaka 2010 na ukweli wa mambo hayo anaujua... “Msigwa anajua kabisa nikiwa kama ‘shipping agent’ (wakala wa meli), sihusiki na kujua kilichopo ndani ya kontena. Wale wanaopaswa kujua ni meneja wa bandari, mamlaka ya mapato, walinzi na wakala wa kupakia na kupakua mizigo, kwa kuwa wao ndiyo wanafanya ukaguzi na kuweka seal (lakiri) …siyo kazi yetu,” alisema.

Alipoulizwa kwa nini hajachukua hatua za kisheria kama anaona amechafuliwa na kama tuhuma hizo hazina ukweli? Kinana alijibu kuwa anajua kuna njia tatu za kuchukua kuhusiana na tatizo hilo lakini bado anazifanyia kazi.

“Kwanza unaweza kujieleza kwenye vyombo vya habari. Pia unaweza kukata rufaa kwa Spika na kesi yako kusikilizwa lakini pia unaweza kwenda mahakamani. Bado natafakari cha kufanya.”

---
Taarifa hi imenukuliwa kutoka kwenye magazeti ya HabariLeo na Mwananchi.
filed under:


Mahakama Kuu ya Tanzania imefuta mashtaka yote ya ugaidi yaliyokuwa yanamkabili Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CHADEMA Wilfed Lwakatare.
 
Taarifa kutoka Mahakama Kuu zinasema Mahakama Kuu imebakiza shitaka moja tu, la utekaji ambalo kimsingi ni Jinai na lina dhamana.
 
Taarifa zaidi zinasema ni shangwe kuu kutoka kwa wafuasi wa Chadema walioko mahakamani na Familia ya Lwakatare.Baadhi ya wafuasi wa Chadema waliohojiwa wamesema huu ni ushindi mkubwa dhidi ya udhalimu.
 
Katika kesi hii Lwakatare anawakilishwa na Jopo la mawakili nguli watano ambao ni Mabere Marando,Tundu Lissu,Professor Abdallah Safari, Peter Kibatala na Naronyo Kicheere.
filed under:

Hii   ni  show  ya  diamond  nchini  Uingereza  alipokuwa  akichambua  na  kulinganisha  mauno  ya  mashabiki  wake
 

 


 

Credit:Florah lymo blog
filed under:
Copyright © 2013 MPEKUZI HURU
WASILIANA NASI KWA EMAIL: mpekuaji@gmail.com