Makonda azindua vitambulisho vya walimu Kupanda bure Daladala Dar


 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (kulia), akimvika kitambulisho Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Turiani, Beatrice Mhina Dar es Salaam jana asubuhi, baada ya kuvizindua vitambulisho hivyo vitakavyotumiwa na walimu kupanda daladala bure wakati wa kwenda kazini kufuatia mpango aliouanzisha wiki iliyopita wa kuwasaidia walimu hao.
DC Makonda akimfika kitambulisho Mwalimu Gideon Mwenenyi.
DC Makonda akimvika kitambulisho, Mwalimu Ramadhani Korowelle.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akizungumza na wananchi na walimu wakati wa uzinduzi wa vitambulisho hivyo.
Ofisa Elimu wa Sekondari wa wilaya ya Kinondoni, Rogers Shemwelekwa (kulia), akizungumza katika uzinduzi huo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Sekondari ya Turiani, Alpherio Nchimbi (kushoto), akizungumza kwenye uzinduzi huo.
Walimu na viongozi wengine wakiwa kwenye hafla hiyo
Wananchi na walimu wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Wananchi na walimu wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Mwalimu Happyness Mailo (kushoto), akimshukuru DC Makonda kwa kuwawezesha mpango huo.
Mwakilishi wa wananchi, Ahmed Muhonga akimshukuru DC Makonda.
Mshairi,  Msafiri Himba akitoa burudani kwenye uzinduzi huo.
Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Turiani, Beatrice Mhina akitoa neno la shukurani kwa DC Makonda.

MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda amezindua vitambulisho vitakavyotumiwa na walimu kupanda daladala bure wakati wakitoka nyumbani kwenda kazini.
Katika hatua nyingine Makonda ameziomba sekta mbalimbali nchini kushiriki katika kutoa mawazo yao ya maendeleo ili taifa lizonge mbele badala ya kuwa watizamaji.
Makonda aliyasema hayo Dar es Salaam jana mbele ya wazazi na walimu wa Shule ya Sekondari ya Turiani wakati akizindua vitambulisho hivyo vitakavyotumiwa na walimu wa wilaya yake kupanda daladala bure kufuatia mpango aliouanzisha wiki iliyopita wa kuwasaidia  walimu hao.
“Nawaomba watanzania na sekta mbalimbali kuwa na mawazo ya maendeleo ambayo yatawekwa mezani na kuyafanyia kazi jambo litakalo msaidia Rais wetu Dk.John Magufuli katika kuliinua taifa kiuchumi badala ya kumuachia kila kitu akifanye yeye” alisema Makonda.
Makonda alitoa mwito kwa makondakta wa daladala kutoa ushirikiano kwa walimu hao kesho wakati watakapoanza kupanda magari yao huku wakijua walimu ndio waliowafundisha na kufikia hatua hiyo ya kazi walizonazo.
Ofisa Elimu wa Sekondari wa Wilaya hiyo, Rogers Shemwelekwa aliwaomba wananchi hao na walimu kuendelea kuunga mkono jitihada za Makonda za kuwaletea maendeleo na kumuombea kwa mungu badala ya kumbeza kwani kazi hizo anazozifanya ni kwa ajili ya wananchi.

Chanzo: GPL


Makonda azindua vitambulisho vya walimu Kupanda bure Daladala Dar Rating: 4.5 Diposkan Oleh: Admin