Msanii Hafsa Kazinja aokoka baada ya kukutana na mauzauza jukwaani

 Hafsa Kazinja
MWANAMUZIKI aliyeamua kumgeukia Mungu na kuokoka, Hafsa Kazinja amefunguka kuwa alikuwa akiteswa na mauzauza ya kishirikina pindi alipokuwa katika majukwaa akiimba Bongo Fleva.

Akipiga stori na paparazi wa Udaku Specially , Hafsa alisema alikumbana na mambo mengi sana ya ajabu ikiwemo kuona majoka makubwa jukwaani akiwa anatumbuiza na sauti za ajabu za mara kwa mara.

“Nilikuwa naishi maisha ya ajabu sana jamani yaani, nikiwa jukwaani naimba basi naanza kusikia sauti za ajabu mara naona majoka makubwa yanapita pita mbele yangu na kunifanya niishiwe pozi katika utumbuizaji wangu, hayo yote najua zilikuwa chuki za binadamu, nashukuru tangu niokoke hivi sasa sina matatizo hayo kabisa,” alisema Hafsa
Msanii Hafsa Kazinja aokoka baada ya kukutana na mauzauza jukwaani Rating: 4.5 Diposkan Oleh: Blog Admin