Mzee Small Afariki Dunia

mzee small
Ni pigo lingine tena kwenye tasnia ya sanaa baada ya kuondokewa na wasanii na kadhaa majuma yaliyopita.

Muigizaji mkongwe hapa nchini, Said Ngamba almaarufu kama Mzee Small amefariki dunia usiku wa leo katika hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa amelazwa akipatiwa matibabu.

Mzee Small amefariki kwa ugonjwa wa presha baada ya kuugua kwa muda mrefu kabla ya kuzidiwa jana na kupelekwa Muhimbili.

Akithibitisha taarifa ya kifo cha Mzee Small, mwanae aitwae Muhidin amesema mzee wake amefikwa na mauti hayo majira ya saa nne usiku wakati akiwa hospitalini hapo akiendelea kupatiwa matibabu.

Mipango inafanyika nyumbani kwao Tabata na kadri taarifa zitakavyokuwa zikitufikia tutaendelea kujulishana.

Mzee Small Afariki Dunia Rating: 4.5 Diposkan Oleh: Admin