Nimeoa, mke wangu amekuwa jeuri na kiburi mpaka nachanganyikiwa

Heshima kwenu wakuu,

Nina mke na watoto wawili na ndoa yangu sasa inakaribia kufikisha miaka 6. Tulipooana tulikuwa tukiishi kwa amani na upendo lakini baada ya kupata mtoto wa pili hali ikabadilika gafla akawa jeuri, majibu ya mkato na kiburi, kila nikijaribu kumsihi na kukaa naye kujadili anatulia siku moja au mbili baadae anarudia kama mwanzo.

Tabia zake zimenifanya niwe mkali na mimi kama kujihami na matatizo haya.

Nilienda kuomba ushauri kwa wataalam wa mahusiano wakaniambia nikae nae tudiscuss na kama anatumia dawa za mpango wa uzazi aziache maana wakati mwingine husababisha hasira za mara kwa mara na wakaniambia pia nichunguze pia labda anaweza kuwa na mshikaj nimejarib kuchunguza hilo nimeona hana.

Pia hata dawa za uzazi wa mpango aliziacha sasa anakaribia miez sita anatumia mbinu za kiasili lakini ktk yote hayo bado habadiliki natamani kuachana nae lkn nawaonea huruma sana wanang wataish ktk mazingira mabaya na hata yeye tumetoka mbali sana nae,pia hata nikiachana nae sitaman kuoa tena, zaid nawaona wanawake wote wako hivyo.

Naomba ushauri wakuu. Asante!
Nimeoa, mke wangu amekuwa jeuri na kiburi mpaka nachanganyikiwa Rating: 4.5 Diposkan Oleh: Unknown